Nyumbani / Habari / Miradi / Mawasiliano

MAJADILIANO NA WANAFUNZI KUHUSU BRN KATIKA WIKI YA SHERIA

Leave a Comment
Katika kipaumbele cha Uboreshaji wa Mazingira ya Biashara katika sekta ya sheria BRN inakuja na mikakati ya kuinua ubora wa utoaji wa haki na utekelezaji wa hukumu

Mtaalam wa sekta ya sheria na BRN kutoka kitengo cha utekelezaji cha Mahakama, Bw, Sebastian Lach akifafanua jambo kutoka kwa wananfunzi wa Shule ya Sekondari Dar es Salaam waliokuwa na shauku kuhusu BRN na waliokuwa wakihoji maswali mazito kuhusu mnufaa ya Mpango huu kwa Taifa.

Meneja Habari na Utetezi kutoka PDB, Bw. Hassani Abbasi akisaidia kufafanua kuhusu nidhamu ya BRN katika kusaidia mabadiliko na mageuzi ya nchi yetu na akifafanua pia kuhusu swali la kijana aliye mbele aliyetaka kujua kama BRN inatekelza visheni ipi ya nchi au ni mpango wa wanasiasa tu!

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Dar es Salaam wakiwa wamevutiwa na kujaa katika Banda la Maboresho ya Mahakama ili kufahamu zaidi kuhusu utekelezaji wa BRN.

Hatimaye majadiliano yaliyokuwa makali yakamalizika kwa furaha huku wanafunzi hawa wakieleza kuikubali BRN na mfumo wake na wakiahidi kuwa mabalozi wa BRN katika shule yao.

Next PostNewer Post Previous PostOlder Post Home

0 comments:

Post a Comment